Katika hali iliyosababisha mshangao nchini Uganda, takribani simba 11 wamekutwa wamekufa kwa kulishwa sumu katika Hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth.
Tukio hili linatajwa kuwa sio tu hasara kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo lakini pia imekuwa shambulio la jitihada za uhifadhi wa simba nchini humo.
Mizoga hiyo ya simba wa kiume 8 na wakike watatu, walikutwa wakiwa wametawanyika katika kijiji cha uvuvi cha Hamukungu, Kusini Magharibi mwa Uganda, wiki iliyopita.
Taarifa ya tukio hili imetolewa na Wizara ya Utalii na Wanyamapori nchini humo na kueleza kuwa simba hao wanafikiriwa kuwa walikula nyama yenye sumu ambayo wamepewa na wanakijiji wa eneo hilo na inawezekana ni kwasababu simba hao walikula ng’ombe wao.
Onyo alilotoa January Makamba kwa Mastaa wa Bongo