Ni Agosti 3, 2021 ambapo mikoa mitatu imezindua rasmi zoezi la kujipatia chanjo ya kujikinga na Uviko 19 (Covid-19) sasa hapa Millardayo.com imekusogezea picha 11 ujionee namna uzinduzi huo ulivyofanyika.
Morogoro
Mkuu wa mkoa Morogoro Martine Shigella leo Agosti 3, 2021 amezindua chanjo ya Uviko 19 uliofanyika katika kituo cha Afya Sabasaba.
Mkoa huo umepokea jumla ya chanjo Elfu 50 Huku mahitaji ni zaidi ya chanjo laki nne Huku vituo 26 vya kutolea huduma hiyo vimetengwa katika Wilaya zote Saba za Mkoa huo.
DODOMA
“Kiujumla Hali ya ugonjwa huu sio nzuri tunazindua leo Chanjo aliye na nafasi akachanje, usisubiri siku watu wakijazana hapo wanaanza kwenda kwenye TV tunaomba Serikali ilete chanjo, hiyo awamu itakuja, kwenye huu wakati ambao unaambiwa kuna chanjo kachanje, huu wakati wengine wanasubiri Mitandao ya Jamii iwaambie wakachanje wewe kachanje, ukisikiliza habari za mitandao ya kijamii anakufa mtu, hali yetu ya Mkoa wa Dodoma sio nzuri tunao wagonjwa kwenye vituo vyetu vya Afya, kwenye mahospitali yetu, tuchukue tahadhari”-Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka
CHANJO YA UVIKO 19 DODOMA YAANZA KUTOLEWA, TAZAMA ILIVYOKUWA
“MZIGO UMESHUSHWA MSIOGOPE, TUNACHANJA CHANJO IKIWA BADO YA MOTO” RC MWANZA