Hizi ni picha za Mchana kwenye Daraja la Tanzanite ambalo limejengwa juu ya bahari kutoka maeneo ya Aga Khan mpaka Osterbay Dar es salaam ambalo tayari magari yameanza kupita rasmi February 1, 2022.
Waziri Mbarawa juzi alikagua Daraja hilo na kutangaza kuanza kutumika kwake baada ya kukamilika kwa 100% likiwa na urefu wa KM 1.03 na upana wa mita 20.5 huku likiwa limegharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 240 na litakua likitumika bure kwa Wananchi wote.
Daraja hili limejengwa na Mkandarasi GS Engineering & Constructiin Corp huku alama za Barabarani kwenye Daraja hilo zikiwa zimechorwa na Kampuni ya Kitanzania ya Stripes n Signs
MUONEKANO WA JUU DARAJA JIPYA LA TANZANITE LINAVYOWAKA, LAANZA KUTUMIKA BURE FEB. 1 2022