Ni miaka miwili ya kulihudumia Jiji na Watu wake, miaka miwili ya kuwaweka Watu kwenye Apartments zenye ubora na usasa, miaka miwili ya kuitendea haki Mikocheni na bahari ya hindi…. Palm Village imekata keki ya furaha na mafanikio usiku wa kuamkia leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi alikuwepo mwanzo mwisho kusherehekea pamoja na Mkurugenzi Jansen wa Palm Village, Wafanyakazi, Wamiliki wa maduka na wageni wengine.
Palm Village Apartments and Shopping Mall ni ‘Kijiji’ ndani ya Jiji la Dar es salaam kinachopatikana Mikocheni kwa Warioba pembeni kabisa ya bahari, Kijiji ambacho hivi karibuni kilitangaza kuuza Apartment zake kwa mkopo wa hadi miaka 20 na malipo ya kidogokidogo kwa miaka mitano kwa wasiotaka mkopo. 📞 0659-800-800