Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la reli Tanzania (TRC) imeadhimia kujenga reli ya kisasa (SGR) kueneza mtandao usiopungua km 2,561 ikiunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na nchi zinazokuwa na bandari (Rwanda, Burundi, DRC).
Reli hii ni ya kisasa na ya kwanza Afrika mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa kwa treni za abiria na 120 kwa treni za mizigo zenye uwezo wa kubeba hadi Tani 10,000 kwa mkupuo.
Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;
1. Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa malori 500 ya mizigo.
2. Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
3. Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
4. Uboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.
5. Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.
6. Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.
Hapa nimekuwekea muonekano wa nje wa stesheni ya Reli ya kisasa ya SGR ambayo kwa asilimia 100% imeshakamilika kwa ujenzi na iko tayari kukupatia huduma pale shughuli za usafirishaji zitakapozinduliwa.
.
RELI YA SGR YAMSHANGAZA RAIS MWINYI “NIMEJIONEA MAMBO MAKUBWA, MIMI NI MKONGWE”
WATOTO WALIVYO ENJOY KUPANDA TRENI YA MRADI MPYA WA SGR UNAOJENGWA NA WATURUKI, MBONI AFUNGUKA
SIRI YA UJENZI WA RELI YA SGR, DR.KIKWETE AFUNGUKA “TULIKWAMA HELA, SIE TUNAONDOKA”