Mnamo Desemba 11, 2022 Mpoto Theatre waliondoka nchini Tanzania kuelekea katika Tamasha kubwa ambalo litafanyika nchini India.
Na leo Desemba 21, 2022 wameanza kuonesha kile walichokiahidi na hapa nimekusogezea picha ushuhudie kile walichokifanya katika Tamasha la kihistoria la kuadhimisha miaka 100 ya Pramukh Swami Maharaj lililofanyika huko nchini India.
“Ningependa Kutoa shukrani za dhati kwa jamii yote ya Hindu wametupokea vizuri maandalizi yamekuwa mazuri, pili tunatoa shukrani kwa Mjomba Mrisho Mpoto kuthamini na kutambua vipaji vyetu na kutoa hii ajira”- Msemaji wa Mpoto Theatre
“Tumekuja katika Tamasha la kihistoria lakini hapa kuna mataifa mbalimbali duniani na jamii yote ya wahindu kwahiyo hii ni fursa kwetu kwa kuja kutangaza kile kilichopo nyumbani Tanzania shukrani za mwisho ziende kwa Rais Samia kwani bila safari ya Royal Tour nafasi hii tusingeipata hivyo filamu imeitambusha vyema Tanzania na leo hii tumepata fursa kama hii asante Mama, asante Mrisho Mpoto tuthamini vya nyumbani”- Msemaji wa Mpoto Theatre