Ujenzi wa barabara kilomita 51.2 unaojengwa kwa kiwango cha lami katika mji wa Serikali MAGUFULI CITY uliopo mtumba jijini Dodoma umefika asilimia 70 na mkataba wake ni shilingi bilioni 89.1 na matarajio ya mradi ni julai 31 na barabara hizo zinatarajiwa kuwa na vituo 52 vya daladala Katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe amelikataa ombi la mkandarasi la ongezeko la muda wa miezi 10 na amemuelekeza mkandarasi mshauri,wakala wa barabara mjini na Vijijini TARURA na meneja wa mradi aliyemteua kusimamia kwa hatua iliyosalia Mhandisi Gilbert Moga kupitia upya ombi hilo.
KWA MARA YA KWANZA WATANZANIA WAMEBUNI MFUMO WA KISHERIA, WAZIRI KABUDI ATOA KAULI “NIMEJIUNGA”