Mwandishi na mtangazaji maarufu wa Uingereza ambaye amewahi kufanya kazi pia CNN Piers Morgan kwa mara nyingine amemponda mke wa rapper Kanye West, Kim Kadarshian kwa kitendo cha kupiga picha za uchi akisema anapiga picha hizi kwa sababu ya tamaa ya fedha na umaarufu na sio uhuru wa mwanamke kama alivyojitetea.
Piers Morgan aliandika kwenye Twitter kwamba Kim Kadarshian angekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake wote ulimwenguni kama angedhihirisha kuwa umaarufu na mafanikio yake vimepatikana akiwa amevaa nguo badala ya kukaa uchi na kuonyesha ishara ya matusi kwa picha ya kidole cha kati.
Morgan amesema Kim na wale wote wanaomuunga mkono akiwemo mwanamitindo Emily wanapiga picha za uchi kwa sababu ya fedha na umaarufu na si harakati za kuwapa nguvu Wanawake na kuwanyanyua toka katika unyanyasaji wa mfumo dume.
Piers morgan amekuwa mpinzani mkubwa wa kitendo cha Kim Kadarshian kupiga picha za uchi akiitazama hii kama harakati ya kujiongezea umaarufu na fedha tofauti na kim anayejitetea kwa kusema kuwa anafanya hivi kuwapa Wanawake uhuru na kujiamini katika miili yao.