Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Kuhusu miili na viungo vya Binadamu vilivyogundulika July 21 Dar es salaam.

on

newssTaarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa.

Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta mamia ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo,baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.

Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Tunaendelea na juhudi za kusikiliza tamko kutoka kwa Jeshi la Polisi juu ya undani wa taarifa hizo,endelea kutufatilia kupitia millardayo.com.

 

Tupia Comments