Unakumbuka ile Stori ya askari Asuma Mpaji na Veronica Nazaremo kufukuzwa kazi Mkoani Kagera baada ya picha zao kusambaa mitandaoni wakionekana kupigana mabusu? safari hii nakuletea tena stori inayofanana na hiyo ambayo imetokea Nchini Uingereza.
Polisi wa nchi hiyo ya Uingereza waliamua kumshtaki mwenzao baada ya kufanya kitendo cha kudhalilisha jeshi la nchi la nchi hiyo kwa kufanya tendo la ndoa tena mbele za watu akiwa na sare za kazi.
Kitendo hicho kimemfanya kufukuzwa kazi bila kupewa taarifa za awali haraka baada ya kwenda kwenye shughuli zake za kila siku za usalama na kufanya kitendo hicho huku akijua ni kinyume na sheria tena akiwa amezungukwa na watu.
Msaidizi mkuu wa kituo hicho, Russ Middleton alisema wanaamini hatua hiyo itakua fundisho kwa wengine kutokana na kitendo cha kulidhalilisha Jeshi.
Polisi mwingine Paraguay naye amekumbwa na mkasa unaofanana na huo baada ya kusambaa kwa picha akicheza na mwanamke ambaye hakuwa amevaa nguo yoyote katika kituo cha Polisi.
Picha ya askari huyo zilinaswa na mitandao mbalimbali ya kijamii huku baadhi ya watu wakiandika kwamba ni kawaida kwa askari wa kituo hicho kufanya vitendo vya aina hiyo na wasichana hivyo kuvuja kwa hii itakuwa ni funzo kwao.
Polisi wanaendelea na uchunguzu huku kesi ya askari huyo ikiwa inaendelea Mahakami.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook