AyoTV na millardayo.com zimepata nafasi ya kukaa kwenye meza moja na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Mohammed Mpinga ambaye amekubali kutoa ufafanuzi kwa Watanzania kabla kamatakamata haijashika mwendo kwa waliofunga taa za ziada kwenye magari.
SPOTLIGHT ZINAZOKUJA NA MAGARI
‘Hizi spotlight ambazo zinakuja na magari zimekua zikitumika vibaya na Madereva na mbaya zaidi ni pale ambapo Madereva au Wamiliki wamekua wakiweka pia kwenye magari yao balbu na Busta zinazopelekea mwanga kuwa mkali zaidi’
‘Mwanga mkali unamfanya Dereva anaemulikwa kuwa na uwezekano wa kusababisha ajali, kimsingi hata yale Magari ambayo yamekuja na taa toka kiwandani bado tunasisitiza yatolewe sababu ni kinyume na sheria ya usalama barabarani kifungu cha 39 c’
‘Nisisitize hasa kwa magari madogo ambayo nayo wakati mwingine yanakuja na spotlight kutoka kiwandani tumeona matumizi yake wakati mwingine yanakua ni maalum, kwa hayo magari tumesisitiza swala la kuzifunika taa hizo kwahiyo kama gari dogo ina spotlight na zimefunikwa sio kosa’
KUHUSU FOG LIGHT ( TAA ZA UKUNGU NA MVUA)
‘Kuhusu zile taa maalum kwa ajili ya ukungu (Fog light) mara nyingi zinakaa chini kwenye Bampa, zile kimsingi hatuzikataza sababu ni maalum kwa ajili ya ukungu au mvua ambapo huwa zinatumika kwa ajili ya kuongeza uono wa Dereva’
KUHUSU TAA NDOGONDOGO:
‘Day light LED, hizi mara nyingi sana tunasisitiza kwa zile ambazo zinakuja na magari toka kiwandani ina maana zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kuweza kuonekana kirahisi barabarani hizo hatujasema zitolewe’
‘Zile Taa za kuongezwa zile ndogondogo zinakaa tatu au nne ndio Marufuku na tumeshuhudia zikiwekwa kwenye Pikipiki na Bajaji na zinaleta kero, zina mwanga mkali ambazo zinaumiza Madereva wengine’
KUSIKILIZA ZAIDI MAAGIZO YA KAMANDA MPINGA BONYEZA PLAY KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
ULIPITWA? Kuna mambo matano ya kufahamu kama una gari lenye Tinted Tanzania, bonyeza play hapa chini kujua zaidi