Mix

Mambo matatu yaliyosemwa na Polisi Geita kuhusu kumkamata Edward Lowassa

on

Jioni ya January 16 2017 ripoti kutoka Geita kanda ya ziwa zilithibitisha kwamba Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa amekamatwa na Polisi akiwa anakwenda kwenye mkutano wa CHADEMA hukohuko Geita ambapo baada ya kusambaa kwa taarifa hizo na baadae kuachiwa, Polisi Geita imeyasema haya baada ya kuhojiwa na millardayo.com na AyoTV.

1:Hatukumkamata Edward Lowassa bali tulikua tumemshikilia tu huyu bwana, na sababu kubwa kabisa za kuwa nae ni swala zima la ulinzi na usalama’Kamanda wa Polisi Geita

2:Usalama wa aina gani…… ni usalama wa kwake yeye kama yeye lakini pia na jamii inayomzunguka, hiyo ndio hoja kubwa iliyokua imejitokeza

3:Polisi haikuwa na taarifa yoyote ya Edward Lowassa kuelekea kwenye mkutano wa CHADEMA, na wakati tumemshikilia tulikaa nae mpaka tulipomaliza mahojiano yetu na ndipo tulipomruhusu akaendelea na safari yake

Unaweza kutazama video ya taarifa ya kukamatwa kwa Edward Lowassa iliyoripotiwa na AzamTV hapa chini

VIDEO: Jeshi la Magereza lilivyoonyesha uwezo wao mbele ya Waziri wa mambo ya ndani tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments