Polisi Dar es salaam imeanza kuingia mtaani kukamata wanaokiuka agizo la marufuku ya uvutaji/uuzaji wa shisha lililotolewa na Waziri mkuu Majaliwa pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema ‘tunaendelea na ukamataji wa wale wanaotumia Shisha ambayo tumebaini inaongezwa vitu vingine kama bangi na unga wa dawa za kulevya‘
‘Mpaka sasa tumekamata watu wawili na tunaendelea kuwahoji, tunaendelea kufanya oparesheni kubwa na kuna wengine wameamua kutoka kwenye mahoteli na kuamua kufanya biashara hii kwenye majumba yao kwa siri, tumeshapata taarifa za hayo majumba, tutafanya mitego na kuwakamata‘ – Kamanda Sirro.
UMEPITWA NA HIZI? WATEULE 185 WALIOMNYIMA USINGIZI RAIS MAGUFULI? MFANYABIASHARA WA MILIONI MBILI KILA DAKIKA JE? BONYEZA PLAY KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI