Ishu za Viwanja vya Shule kunyang’anywa na watu alafu wanafanyia shughuli nyingine badala ya kuweka viwanja vya michezo ni moja ya vitu ambayo nimevisikia mara nyingi kwenye mijadala ya Bunge.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa Mwanza ambako alikuwa akifanya uzinduzi wa michezo ya UMISETA ambayo inafanyika Mwanza.
Kagusia ishu hiyo: “Michezo inahitajika sana katika jamii yetu.. Serikali lazima tuendelee kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa Michezo.
Maeneo mengi unakuta kuna migogoro ya maeneo ya Shule kuchukuliwa na watu katika miji yetu, huu ni udhaifu kwa idara ya mipango miji hakuna sababu ya hili kutokea.
Wakuu wa Mikoa muhakikishe kila Shule na maeneo yake yanapimwa na yapewe hati ili kulinda kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali, tusipofanya hivyo migogoro ya ardhi haitapungua hata kidogo“>>>– Waziri Mkuu Pinda.
Hizi ni baadhi ya PICHAZ toka Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza wakati wa uzinduzi wa Michezo hiyo.
Hapa iko sauti ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda alivyokuwa akiongea kwenye Uzinduzi huo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.