Kikao cha Bunge kikaendelea leo Dodoma, Waziri Mkuu alipata nafasi kuzungumzia mengi ikiwemo hizi ishu mbili ambazo zilichukua headlines kubwa kwenye vyombo vya habari, kwanza ni maafa ya mafuriko na pia ishu ya Mawaziri waliohusika na ESCROW kusafishwa.
Kuhusu ishu ya maafa ya mafuriko Dar >>>“Watanzania lazima tubadilike.. lazima wakati mwingine tukubaliane na ushauri wa Serikali, kelele za watu wanaoishi mabondeni hazijaanza leo nakumbuka tangu enzi za mzee Makamba ilifika mahali anashika sululu anakwenda kubomoa mwenyewe”– Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“Wale wote walioko mabondeni haiwezekani kila mwaka kazi yako ikawa ni kuhama na ukichelewa maji yakukute lawama kwa Serikali, itafika mahali Serikali itasema imechoka.. tokeni mabondeni kwa hiari yenu wenyewe”
Haya ni majibu kuhusu Mawaziri ‘waliosafishwa’ >>>Taarifa ya Baraza la Maadili baada ya kupitia mchakato wake kwa misingi ya maadili haiwaondolei uwajibikaji.. Mamlaka ya hawa wote ni Rais mwenyewe.. taarifa ilitolewa wakati yuko nje ya nchi, bado mwenye kauli ya mwisho ni Rais mwenyewe atakuwa na uamuzi wa mwisho nini kifanyike>>> Waziri Mkuu Pinda.
>>Wale ambao Tume ya Maadili waliona wana kesi ya kujibu wanaendelea nao.. niliona Magazeti wameandika Ikulu imewasafisha, sio kweli kwamba Ikulu imewasafisha..>>>
Hapa Waziri Mkuu Pinda akawagusia UKAWA nao kujenga shule au Zahanati >>>Mheshimiwa Mbowe.. Nangoja siku moja niwaone UKAWA angalau mchangishe pesa mjenge shule hata moja tu basi au Zahanati moja, itatia moyo sana>>> Waziri Mkuu Pinda.
Ukiplay hapa utamsikia akiongelea ishu hizo zote…
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.