Kutokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini, leo August 25 2016 Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya kivyama ndani na nje ili kuzuia machafuko ya amani yanayoendelea kujitokeza katika kipindi hiki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Kamishna wa Polisi CP Nsato Marijani amesema…>>>’Jeshi la polisi halikuzuia mikutano ya ndani ya siasa kwasababu tulikuwa tunaamini ni mikutano iliyokuwa ikizungumzia maendeleo ya wananchi‘
‘Lakini sasa tumebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kucchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la polisi‘ –CP Nsato Marijani
‘Kwasababu hiyo basi kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani‘ –CP Nsato Marijani
ULIIKOSA HII ALICHOKIONGEA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA KUFIKA ENEO WALIPOUWAWA ASKARI POLISI