Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamshikilia ofisa programu wa kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti pamoja na watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano zaidi.
“Polisi Kanda Maalum ya DSM tunamshikilia Tito Magoti (26), Mkazi wa Ubungo Kibo, Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( LHRC ) pamoja na Watu wengine watatu kwa uchunguzi na mahojiano kwa tuhuma za makosa ya jinai, Tito hajatekwa”- MAMBOSASA