Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa Viongozi wanaohamasisha mikusanyiko ya watu isiyo zingatia sheria za nchi na yenye lengo ovu kwa taifa.
Kauli hii imetolewa leo kufuatia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanaohamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kukusanyika kwenda kumpokea mmoja wa wanachama wao anayetarajia kuwasili nchini Tanzania kwenye uwanaja wa Mwl. Nyerere July 7, 2020.
Jeshi la Polisi limesema linatambua watanzani wapo kwenye kipindi cha maombolezo lakini hilo halitawazuia kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria wale wote wanaokusudia kufanya mikusanyiko bila kuzingatia sheria.