June o7 2016 Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa inayosema kwamba wamepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).
Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao. Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.
kupitia taarifa hiyo Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia June 07 2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
Jeshi la Polisi limewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha taarifa hiyo imewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
ULIKOSA WALIYOYAZUNGUMZA CCM BAADA YA UPINZANI KUSEMA WANAENDA KWA WANANCHI KUSHITAKI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE