Kumekuwa na ishu ya kuvuja kwa picha za utupu za watu mbalimbali ikiwemo mastaa kwenye mitandao, wakati mwingine tumesikia wenye picha hizo wakilalamika kwamba zimevujishwa na wapenzi wao wa zamani.
Kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya aina hii, Uingereza wamepitisha Sheria, iwapo ukivujisha picha za utupu za mtu yoyote bila idhini yake ni kifungo cha miaka miwili pamoja na faini.
Kwa Marekani hii Sheria imepitishwa kwenye majimbo 12 tayari.
Ishu za kuvujisha picha, video zipo hata Bongo pia, unadhani ikipitishwa Sheria itasaidia kukomesha hii? Unaweza kuniandikia comment yako kwenye hili mtu wangu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook