Baada ya kuhairishwa kwa Bunge la maalum la Katiba,Bunge la bajeti linaanza leo Mei 06 Dodoma ambapo wabunge wanatarajiwa kuanza kulipwa viwango vipya vya posho ambapo itakua ni shilingi 300,000 kwa siku ambayo ni sawa na viwango sawa na walivyokuwa wakilipwa wajumbe bunge maalum la katiba.
Kabla ya kupandishwa kwa posho hizo Wabunge walikua wakilipwa 200,000 kwa siku ambayo mgawanyo wake ulikua ni sawa na 70,000 kama posho ya kikao 80,000 posho ya kujikimu na 50,000 gharama za usafiri ambapo nyongeza hiyo ya kila mbunge ambayo ni sawa na asimilia 50 itaigharimu serikali Tsh Bilioni 18.5 kwa siku 52 zilizotengwa kwa ajili ya bunge hilo la bajeti.
January 2012 Rais Jakaya Kikwete alikataa maombi ya bunge ya kutaka nyongeza ya posho ipande hadi laki tatu na thelathini na badala yake Wabunge hao wakapata nyongeza ya elfu 50 tu kwa ajili ya usafiri.
Bunge hili linategemea kumalizika June 27.