Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM The Peoples Station umekupita? Ninazo zote kubwa za leo tarehe 12 October 2015 kwenye kurasa za magazeti… karibu uperuzi na hizi nyingine kama zilikupita.
Mzee Mkapa choppa nne kumnadi Magufuli, Musoma wasafisha barabara kumkaribisha Lowassa, Rais Kikwete aitaka TANESCO kutafuta njia ya dharula ya kuondoa kero ya umeme, Magufuli kuanza kazi, Uchaguzi mwaka 2015 changamoto kubwa… Magufuli ataja nguzo zake kumi baadhi zikiwa, kuongeza mapato ya serikali, kurekebisha Sheria zenye mapungufu, kupendekeza njia za haraka kuondoa kero za walimu na madaktari na kutimiza nguzo ya elimu ya kila kijiji.
Baadhi ya wachambuzi wamesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2015 ni wa kihistoria kutokana na wananchi kutambua wajibu wao kwa muamko mkubwa, na uwezekano wa kutaja Chama kipi kitashinda umezidi kuwa mdogo kutokana na kila mtu kunandi ushindi wa Chama chake.
Mzee Kingunge amesema historia itamuhukumu baada ya kuhama CCM kutokana na uvunjwaji wa kanuni ndani ya Chama hicho huku January Makamba amshambulia Mzee Kingunge na kusema kuwa ni mtu ambaye amepotoshwa na rushwa huku uamuzi wake wa kuhama Chama hicho baada ya miaka 61 inadhirisha wazi udhaifu wake.
Viongozi wa vyama vya Siasa wanatakiwa kunadi sera zao na sio kasoro za wagombea kwani vitendo hivyo vinachochea uvunjaji wa amani… CCM kimeongeza nguvu kwenye kampeni zake za Lala Salama kwa kumuongeza Mzee Mkapa ili kumnadi mgombea wa Chama hicho Dk. John Magufuli.
Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa jana alipokelewa na umati mkubwa wa watu mjini Musoma waliofagia na kudeki barabara ili mgombea wao asipatwe na mafua wakati anahutubia kwenye mkutano wake… Kiwanda cha cement cha DANGOTE kilichopo Mtwara kimezinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete na kinatarajia kutoa ajira kwa watu 1500.
Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast nimeirekodi na kukuwekea hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.