Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee maarufu pia kama Vee Money anaziandika headlines jumatatu hii kwenye kurasa za burudani!
Baada ya single yake mpya ‘Never Ever’ kutambulishwa kwenye Trace Nigeria, Vanessa, Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz wakaendelea kuipepersuha vizuri bendera ya Tanzania kwenye tuzo za AFRIMMA Awards 2015 zilizofanyika weekend iliyopita jijini Dallas, Texas… ambapo Vee Money alibeba ushindi wa Tuzo moja ya Best Female East Africa!
Good news mtu wangu, kama wewe ni shabiki wa Vanessa Mdee na pia ni shabiki wa muziki mzuri basi hii news ikuguse popote pale ulipo… single mpya ya Vanessa Mdee ipo hewani tayari na imeshafanyiwa video, kama hukubahatika kabisa kukutana nayo siku iliyokuwa inazinduliwa kwenye Trace Nigeria basi karibu uitazame video hiyo hapa chini kwa mara ya kwanza!
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE.