Duniani

Pale ambapo mtuhumiwa ameamua kuwatumia Polisi selfie yake ili wamtafute vizuri.

on

Ikitokea unakutana na ripoti kwenye kona yoyote kwamba unatafutwa na Polisi lazima mapigo ya moyo yaanze kwenda kasi… kama ni kesi, unatafutwa kwa kesi gani? Hilo swali halitokosa kujiuliza, lakini jamaa wa Marekani kaona isiwe tabu, hajapenda picha yake ambayo Polisi wameitumia kutangaza sura yake kwamba anatafutwa, akatwanga selfie yake alafu akawatumia Polisi.

Kwa ujasiri wake wote na kuonesha kwamba hakuwa anatania akaamua kuwaandikia kabisa >>> ‘Picha hii iko poa zaidi kuliko hiyo mliyotumia

Jamaa huyo Donald “Chip” Pugh kwa bahati nzuri alipatikana kwa njia ya simu akafanyiwa interview kwenye radio moja, akalalamika kwamba picha waliyotumia Polisi ni ya ovyo kabisa wala hakuipenda… walipomuuliza yuko maeneo gani jamaa akagoma kabisa kujibu.

Donald kutoka  Lima, Ohio Marekani alikuwa na kesi na alitakiwa kuripoti Polisi, lakini kwa sababu hakutokea Kituo cha Polisi, jamaa wakaweka picha yake kwenye ukurasa wa Facebook ambayo yeye hakuipenda, akapiga selfie akawatumia ili waitumie hiyo kutangaza wanamtafuta.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments