Moja kati ya habari kubwa iliyokuwa inasambaa katika mitandao ya kijamii ni pamoja na habari za club ya Arusha United ya jijini Arusha, kutaka kujiondoa katika kushiriki michuano ya Ligi daraja la kwanza Tanzania kwa madai mbalimbali.
Arusha United ilitangaza kuwa itajitoa endapo TFF haitachukua hatua za haraka kuhusiana na madai yao yanayoendelea katika Ligi daraja la kwanza, leo Rais wa TFF Wallace Karia mbele ya waandishi wa habari amejibu kuwa club hiyo ipo haijajitoa na imerudishwa kwa wenyewe JKT.
“Kuna maombi ambayo halali na maombi yasio halali kwa mfano mtu akiomba kuua mtu utamruhusu? sisi tunacheza mpira mtu anaomba kuua mpira kwa hiyo tumewakatalia na ile timu kuna mahali waliitoa, tulivyowakatalia wametuletea barua kuwa wameikabidhi kwa wenyewe JKT walipoichukua”>>> Wallace Karia
Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys