Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia ameongea na vyombo vya habari leo kuhusiana na maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON U-17 yatakayofanyika Tanzania kuanzia April 14 2019 katika viwanja vya Chamazi na Taifa.
Kuelekea michuano hiyo Rais wa TFF Wallace Karia amemuomba mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kupitia kamati yake ya kuhamasisha Taifa Stars ishinde, kuhamishia nguvu kwa kuisapoti Serengeti Boys ishinde michuano ya AFCON U-17 na kufuzu kucheza fainali za Kombe la dunia la vijana.
“Nilimuomba Rais Magufuli kuwa mbali ya kuwa RC Makonda ana majukumu mengi kwa kazi yake ya mkuu wa mkoa lakini nilimuomba kuwa aendelee kutusaidia, angalau yeye na kamati yake waweze kuendelea kwenye mashindano hayo ya AFCON U-17 kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano hayo”>>> Rais wa TFF Wallace Karia
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars