Mgombea wa Chama cha Upinzani nchini Sierra Leone, Julius Maada Bio ameamua kufanya shughuli ya kuapishwa kuwa ‘rais’ wa nchi hiyo hotelini, ikiwa ni saa chache baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu.
Bio ambaye amewahi kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi kifupi mnamo mwaka 1996, ametangazwa kumshinda kwa kura chache mgombea wa chama tawala Samura Kamara.
Bwana Bio aliapishwa chini ya saa mbili baada ya kutangazwa mshindi. Mgombea Kamara ameeleza kuwa atakwenda kufungua kesi mahakamani kwa madai ya makosa mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi.
Agizo la Waziri Nchemba kwa Jeshi la Polisi “msiwaachie”