Ni headlines juu ya headlines kutoka +254 Kenya kwa Uhuru Kenyatta ambapo muda huu nakusogezea stori kumhusu Mbunge wa Jimbo la Ruaraka nchini Kenya aliyehusika katika kiapo cha kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ameachiliwa kwa dhamana ya Tsh.1106198 baada ya kulala mahabusu ya Kiambu toka alivyokamatwa Jumatano.
Tom Kajwang alifikishwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi leo February 1, 2018 ambapo alitarajiwa kukabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kushiriki katika mkutano wa kula kiapo kwa Odinga kinyume na sheria.
Wabunge wa NASA waliojaa katika mahakama hiyo walisema kuwa mashtaka aliyofunguliwa Kajwang ni bandia. Hata hivyo kesi yake itaendelea tarehe 6 February 2018.
Mbunge huyo ambaye alisimama nyuma ya Raila wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika uwanja wa Uhuru Park Jijini Nairobi alikamatwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi na kupelekwa makao makuu ya ujasusi ili kuhojiwa.
CHADEMA WANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA.