Top Stories

Vikundi vyajitokeza ‘kum-support’ Jacob Zuma Makahamani

on

Vikundi mbalimbali nchini Afrika Kusini ikiwemo vya kidini vimeandaa mkesha maalumu utakaofanyika usiku wa April 5, 2018 Jijini Durban kama ishara ya kuwa nyuma ya Rais Mstaafu wa nchi hiyo Jacob Zuma anayetarajia kupandishwa kizimbani.

Wafuasi hao wameandaa mkesha huo saa chache kabla ya Zuma kufikishwa Mahakama Kuu ya KwaZulu Natal kujibu mashtaka 16 ya ubadhirifu, rushwa na utakatishaji fedha ambayo yanahusishwa na malipo 783.

Malipo hayo yanadaiwa kufanywa kwa kuhusishwa na biashara ya silaha ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya mabilioni ya Rand (aina ya pesa) ya nchini humo.

Mwenyekiti wa Chama cha Maveterani wa Jeshi wa chama cha siasa cha ANC Kebby Maphatsoe amesema atahudhuria kesi hiyo kwani amejifunza kusaidia rafiki wakati wa dhiki.

Mrisho Mpoto amwambia Steve Nyerere “Punguza gubu ndugu yangu”

Soma na hizi

Tupia Comments