April 21 kila mwaka Malkia Elizabeth II wa Uingereza husherehekea siku ya kuzaliwa ambapo mwaka huu yaani April 21, 2017 ametimiza miaka 91, na kwa kuwa siku maalum kwake nimeona nikuletea sheria ambazo Malkia huyo anaweza asizifuate na hawezi kutiwa matatani.
1: Kuendesha gari bila leseni
Kosa la kuendesha gari bila leseni nchini Uingereza adhabu yake ni kifungo na kulipa faini kwa pamoja, lakini sheria hii haimbani Malkia wa nchi hiyo kwani ana uwezo wa kuendesha gari bila ya leseni.
2: Uwezo wa kusafiri nchi yoyote bila passport
Hii inaweza kukushangaza, lakini ukweli ni kwamba Queen Elizabeth II anaruhusiwa kusafiri nchi yoyote duniani bila kuwa na passport.
3: Halipi kodi
Kwa kawaida Marais na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani hulipa kodi kama wananchi wengine ili kuweka usawa kati ya viongozi na wananchi, lakini ni tofauti kwa Malkia wa Uingereza ambaye anaruhusiwa na Katiba ya nchi hiyo kutokulipa kodi ingawa aliamua mwenyewe kulipa tangu mwaka 1992.
4: Hawezi kupelekwa Mahakamani
Miongoni mwa vitu vinavyoonesha uwepo wa haki, usawa na utawala bora katika nchi ni pale kiongozi yoyote wa serikali kushtakiwa anapomaliza muda wake, lakini kwa Malkia wa Uingereza haruhusiwi kushtakiwa au kupelekwa Mahakamani hata kwa kuua.
5: Anaruhusiwa kuendesha gari kwa speed kali
Wananchi wa Uingereza wanatakiwa kuendesha gari kwa speed ya 70 mph iwapo mtu atakamatwa akiwa anaendesha gari kwa speed kubwa zaidi ya hiyo iliyobainishwa na sheria, adhabu ni kifungo na faini kwa pamoja, lakini Malkia wa Uingereza anaruhusiwa kuendesha gari kwa speed anayoitaka yeye.
VIDEO: Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu mashabiki wa mpira kuweka vitu rehani? Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo