Habari za Mastaa

‘Nilishawahi kulipa kiingilio Kumbi za Starehe nipate nafasi ya kuimba’ – Timbulo

on

Watu wangu wanaopenda kufuatilia maisha ya mastaa na muziki wa Bongo fleva ninayo stori hii ambayo inamuhusu staa wa muziki huo Timbulo ambaye anatamba na wimbo wa Mfuasi.

Leo April 21, 2017 Timbulo ameweka wazi kuhusu maisha yake ya muziki akisema kuwa alishawahi kulipa kiingilio kwenye kumbi za starehe ili apate nafasi ya kuimba ili ajulikane kirahisi huku akisema anaamini sana kwenye wakati kijua kuwa wakati ukifika basi umefika.

Akizungumza kwenye XXL ya Clouds FM wakati wimbo wake ukiwa jiwe la wiki alisema:>>>”Nilishawahi kulipa kiingilio kumbi za Starehe nipate nafasi ya kuimba. Wanione nikiwa sijawahi kutoa wimbo. Siku zote mimi ni muumini wa wakati. Ipo siku itafika, na nikiona inafikia hatua kuwa milango kama hivi inafunguka mpaka Dozen ananiita ‘njoo jiwe la wiki’ naona kaielewa ngoma. 

“Kuna mabadiliko nimeyafanya kutoka kwenye ‘Usisahau’ ambao wenyewe ulikuwa jiwe la wiki kipindi cha nyuma na ikumbukwe kuwa ‘Mfuasi’ ndio wimbo wa kwanza kutambulishwa kwenye XXL. Kwa hiyo, vitu vinafunguka vyenyewe tu.” – Timbulo.

VIDEO: Ayo TV imekutana na msanii Lulu diva akiwa South Africa ana haya yakutueleza. Bonyeza play kutazama. 

Soma na hizi

Tupia Comments