Michezo

PICHA: Frank Domayo ameipeleka Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017

on

January 10 2017 Azam FC walishuka dimba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan, Azam FC ambao wanakumbukumbu ya kupata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Yanga mchezo uliyopita, leo wametinga fainali kwa ushindi wa goli 1-0.

Ushindi wa Azam FC uliyowapeleka fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2017, ulipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 33 baada ya Frank Raymond Domayo kupachika goli la ushindi ambalo ndio lilidumu kwa dakika zote 90.

whatsapp-image-2017-01-10-at-19-52-33

Mchezo wa Azam FC umechezwa huku kocha wao mpya Aristica Cioaba aliyekuja kurithi nafasi ya Zeben Hernandez akiwa jukwaani, akishuhudia vijana wake wakitinga fainali ya michuano hiyo, ambapo watakuwa wakimsubiri mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments