Siku moja baada ya Kamati ya saa 72 kupitia Mwenyekiti wake Hamadi Yahaya kutangaza kuwa Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, leo Yanga wamefanya mkutano na waandishi wa habari.
Yanga wamefanya mkutano na waandishi wa habari kupitia mjumbe wao wa Kamati ya Utendaji Salum Mkemi na kueleza kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati hiyo, hivyo wameeleza msimamo wao kwa sasa baada ya Simba kupewa point tatu na magoli mawili.
Kutokana na maamuzi hayo Yanga wamekumbushia rufaa yao dhidi ya African Lyon ya kumchezesha mchezaji Ludovic Venance akiwa bado anatambulika kama mchezaji wa Mbao FC ya Mwanza, rufaa ambayo bado haijatolewa maamuzi hadi sasa.
VIDEO: Simba ilivyobadilisha matokeo vs Mbao FC dakika za mwisho Mwanza