Mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga Salum Mkemi kwa niaba ya kamati yao wanaipinga rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa madai ya kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano katika mchezo wa Simba dhidi ya Kagera April 2 uliyomalizika kwa Simba kupoteza kwa goli 2-1
Yanga wanasema mchezaji Fakhi anayekatiwa rufaa amekubali kuwa ana kadi tatu za njano lakini mbili za VPL na moja ni kadi ya FA hivyo hazihusiani na ilikuwa halali kucheza katika mchezo dhidi Simba, Yanga wanahisi Simba wanafanya udanganyifu ili wapate point za mezani na kuitoa Yanga kileleni.
Simba na Yanga zimetofautiana point mbili Simba akiongoza kwa kuizidi Yanga point mbili ambapo Simba wana point 58 na wameizidi Yanga mchezo mmoja hivyo wanaipinga rufaa ya Simba dhidi ya Kagera kwa kigezo kuwa inawagusa moja kwa moja na kamati itakayoamua ina tuhumiwa kuwa na watu wa Simba.
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017