Mtanzania Mbwana Samatta ambaye kwa sasa Tanzania ina mtazama kama balozi wa soka la Tanzania barani Ulaya akiwa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji, ameonekana kuwa na tabia ya kupenda kushea vitu vya kitanzania na wachezaji wenzake wa KRC Genk.
Ikiwa ni siku moja tu imepita toka Samatta ampost Jean Boetius raia wa Uholanzi anayecheza nae katika club KRC Genk ya Ubelgiji akisoma Kiswahili, leo Samatta amempost tena Jean Boetius akisoma lugha ya Kiswahili, wakati huu akisoma ujumbe wa pongezi kwake baada ya kusoma vizuri mara ya kwanza.
Kama hufahamu vizuri Jean Boetius ni staa wa soka wa kimataifa wa Uholanzi aliyejiunga na KRC Genk kwa mkopo mwaka huu akitokea club ya FC Basel ya Uswiss, Boetius ni mbadala wa Leon Bailey aliyeihama KRC Genk mwaka huu na kujiunga na Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Jean Boetius raia wa Uholanzi anayecheza na @samatta77 KRC Genk ya Ubelgiji anaendelea kujifunza lugha ya Kiswahili #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/ePLdQhuEvC
— millard ayo (@millardayo) April 15, 2017
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera Sugar leo April 2 2017