Moja kati ya habari inayosambaa katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni pamoja na habari za wachezaji wa club ya Dar es Salaam Young Africans kudaiwa kuingia katika mgomo wa kufanya mazoezi kwa siku ya pili mfululizo kwa madai ya viongozi wao kuwapuuzia.
AyoTV imeongea na katibu mkuu wa Yanga Omary Kaya na ameongelea suala hilo kuwa, halikuwa na mgomo wowote zaidi wachezaji wao walikuwa wanataka kupata ufumbuzi kutoka kwa viongozi waliopo baada ya kuona kuna baadhi ya mambo yanaendelea mitandaoni.
“Kwanza kabisa niseme sio mgomo mtu akiwa na mgomo hawezi kuja katika eneo lake la kazi na sasa hivi hapa mimi ninavyoongea nilikuwa natoka katika mazoezi yao kwamba wao walikuwa wanataka kulikuwa kuna mazungumzo walikuwa wanataka ufafanuzi kutoka kwa viongozi kuhakikisha kila kitu kinasonga”>>>Omary Kaya
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23