Michezo

Ujumbe wa James Msuva kwa Simon Msuva baada ya Yanga kupata suluhu vs Mtibwa

on

Moja kati ya matokeo ambayo yamewahuzunisha mashabiki wa Yanga leo ni kushindwa kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar, kwani kama wangepata ushindi leo walikuwa wanapata nafasi ya kuongoza katika msimao wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa tofauti ya magoli dhidi ya Simba.

James Msuva

James Msuva ambaye ni mdogo wa Simon Msuva wa Yanga ametumia ukurasa wake wa instagram kumuandikia ujumbe wa kumfariji kaka yake ambaye katika mchezo huo alipiga penati na kukosa, James ameandika ujumbe huo ambapo dakika kadhaa baadae Simon Msuva alijibu kwa ku-comment.

“Trust Me My Blood Bro;,,,,,Wakat Wewe Ukipanga Lako Kumbuka Mungu Nae Anazidi Kupanga Yake Najua Roho imetuuma sana na wachache watakao Amini hilo Ila sisi Tuzidi KUPAMBANA BRO MDOGO WAKO NIPO BEGA KWA BEGA NA WEWE KWA LOLOTE LITAKALO KUTOKEA LIWE ZURI AU BAYA #mungutusaidie @msuva27@jmsuva10 #kilichokutokea Leo ni sehemu ya kujifunza zaidi” >>> James Msuva

“Ni kweli dogo mimi siwezi choka cause naipenda timu yangu na bado watu wengi wanahitaji msaada wangu, mimi naomba uzima tu naamini Mungu atafungua njia zote zilizofungwa na naamini kwa uwezo wake nafasi bado tunayo na tutapigana mpaka mwisho @jmsuva10 >>> Simon Msuva

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments