Leo Aprili17, 2019 Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ametoa mkopo wa Pikipiki 26 na Bajaji 30 kwa vikundi mbalimbali ukiwa na thamani ya Shilingi Bilioni 1.7 lengo ni kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi ili kuwakwamua na umasikini na kuwaweka uchumi wa kati.
Akizungumzia mkopo huo, DC Mjema amesema hiyo ni awamu ya kwanza na itakapofika Mei mwaka huu watatoa mkopo mwingine ili kufikia Bilioni 2 lengo ni kuhamamisha wananchi kujiunga kwenye vikundi badala ya kila mtu kupewa mkopo wake.
“Wananchi wakumbuke huu ni mkopo na warudishe Pesa ili wengine nao waweze kuchukua mkopo ambapo tunawawezesha wananchi wakiwemo walemavu ili kuwaondoa katika umasikini na kuwaleta katika uchumi wa kati,”amesema