Muigizaji Faiza Ally amerudi tena kwenye headlines leo July 23,2018 baada ya kumuandikia mzazi mwenzake Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu barua ya kumtaka ajitathmini na kutafuta njia sahihi ya kumtunza mtoto wao Sasha.
Kupitia ukuarasa wake wa instagram ameandika barua hiyo na kusema kuwa hapendezwi na yeye kufanya shopping Mlimani City na kusema kuwa ni dharau kubwa hivyo awe na heshima kwake na mwanae Sasha.
“Natuma barua kwako kwa sababu sehemu pekee ya kukufikishia ujumbe ukaupata ni hapa ni hivi toka tumeachana sasha ana mwaka na miezi 6 mpaka leo hujatafuta namna sahihi ya kumtunza mwanao sasa tafuta njia sahihi na yenye heshima mimi sio wa kufanyia shopping na happy eti nikachukue mlimani 😂😂😂”
“Hiyo ni zarau sana baba kama ulikosa muda ungetuma hela ! Lazima uweke heshima kwa baby mama wako na mwanao! sasa ni hivi siwezi kwenda kuchukua sukari na maziwa mlimani ni DHARAU!!!!!!”
EXCLUSIVE: Mtoto wa miaka 9 anaehubiri aongea yote