Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ameagiza vijana 800 wenye shahada waliojitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa miaka miwili kuajiriwa Serikalini kuanzia February, 2020.
Akizungumza Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro amesema Rais Magufuli aliagiza vijana hao wenye kiwango cha shahada waajiriwe Serikalini kwa kuwa wamejitolea kwa muda mrefu hivyo wamejenga uzalendo.
“Katika kipindi cha 2019/20 Serikali imetangaza nafasi 40,000 na ajira zinaanza Februari, lakini cha msingi tutaanza na hao vijana ambao kwa hesabu ya kawaida hawazidi 800 wenye sifa,” Dk. Ndumbaro.
Katibu Mkuu huyo amewataka vijana hao kuandika barua utumishi wakiambatanisha na nakala za vyeti vya taaluma pamoja na uthibitisho wa wakuu wa kambi zao na wakifanya hivyo, watambue kazi wamepata.
Ameonya watumishi ndani ya Serikali ya Tanzania ambao wanaendelea kuwatetea wenzao ambao walioondolewa kwa kuwa na vyeti feki kwamba Serikali itaanza kuwashughulikiwa.
HABARI NJEMA WAZIRI AWEKA WAZI TRENI YA ABIRIA KUTINGA ARUSHA