Mgombea wa ‘Urais’ kupitia Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’, Dkt. John Magufuli ameeleza kuwa Chama hicho kilimetua Charles Kajege kugombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara, badala ya Kangi Lugola.
Rais Magufuli amesema Lugola na Kajege walifungana kura (173), hivyo kutokana na Lugola kuwa Mjumbe wa mkutano, alijipigia kura mwenyewe ina maana wajumbe 172 pekee ndiyo walimchagua.
“Tukasema huyu Lugola ni mtu mzuri namfahamu na makazi Serikalini yapo mengi tu na yeye ametoka ametulia wala hakubabaika, Lugola kula samaki wako vizuri enjoy CCM ipo tu” JPM
“Lugola na mwenzake walifungana, utawapeleka wote kugombea Ubunge?, nikapiga hesabu walipofungana kura zilikuwa 173, tukahesabu nani ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya tukakuta Lugola ni Mjumbe, kwa hiyo kura 1 alijipigia, kwahiyo moja kwa moja, tukitoa hiyo 1 yeye anaondoka” JPM
“WASIMAMISHE WAGOMBEA WANAOTUPA IMANI, MMEMCHAGUA DOGO JANJA” MARIAM DITOPILE