Rais Magufuli amemshukuru Askofu Mkuu Dkt. Mtokambali na Waumini wa Kanisa la TAG kwa tuzo hiyo na ameeleza kuwa tuzo hiyo inamstahili Mwenyezi MUNGU ambaye amesikiliza maombi ya Watanzania na kuepusha madhara ya janga la Corona ambalo limeleta taharuki kubwa duniani.
“Nashukuru nimefika hapa hakuna aliyevaa barakoa, ningeshangaa ni nani Mchungaji asiyetambua nguvu ya Mungu wakati amebeba Biblia, mmethibisha hili, ndio maana nasema nilipoingia hapa nimemuona Mungu yupo hapa, corona tumeishinda tupo salama, tumeyazidi hadi Mataifa makubwa”-JPM
“Nimeona hapa Watumishi wa Mungu kutoka nje ya Nchi na wao hawajavaa barakoa kwakuwa wamemtanguliza Mungu, mkienda kwenye Nchi zenu mkawaambie jinsi Tanzania ilivyoishinda vita ya corona kwa kumuamini Mungu, hii inatufundisha tukipata matatizo tusitegemee akili zetu pekee” -JPM