Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya ambao wakifika kwenye maeneo yao ya kazi wanajiita marais wa eneo hilo. Amesema wanajivisha madaraka yasiyo.
Ndugai ameyasema hayo leo Mei 19, 2021 wakati wa kuapishwa wakuu wa mikoa na viongozi wateule Ikulu jijini Dar es salaam.
”Kuna Wakuu wa mikoa na wilaya huko wanajiona ni Rais, utasikia mimi ni Rais wa mkoa/wilaya hii, nani amesema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais ni Samia Suluhu Hassan basi, huo ndio ukweli” – Spika Job Ndugai.
”Utengenezwe utaratibu wa viongozi kuwajibika kwa pamoja yaani Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi maana haiwezekani jambo likiharibika linakuwa la Mkurugenzi pekee, hawa wengine wana-relax” Spika Ndugai.