Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka ujumbe wa tahadhari kwa Waziri wake wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kufuatia msururu wa madudu unaoendelea katika taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.
“Naomba Waziri (Prof Makame Mbarawa) fanya marekebisho unayoweza. kama huwezi njo tukae kitako, mimi wewe, Katibu Mkuu Kiongozi…
Waziri nilikuweka kwa kukuamini, na ninaomba nenda kasimamie kazi hii kama ninavyo tarajia na utakapo shindwa njoo uniambie dada nimeshindwa nitaangalia mwingine atakayeweza kunisaidia— Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa gati za Bandari ya Dar es Salaam.