Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kongamano la Wanawake wa CHADEMA Mjini Moshi leo amesema kwa ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania ipo vizuri kiuchumi kuliko Nchi yoyote.
“Mengine yote nataka niwaambie kiuchumi tuko vizuri ndani ya ukanda huu wa Afrika Mashariki, tuko vizuri kuliko Nchi yoyote ile msidanganywe, sasa hivi Nchi zinalia na ukata wa pesa za kigeni sisi tuna akiba ya miezi minne, nenda kwa Majirani ya Wiki moja mbele hawana”
“Tunapata maombi ya kuwawekea Watu dhamana mafuta yaendelee kupelekwa kwao lakini na sisi tunajifanya hivyohivyo ‘na sisi jamani hali ngumu hatuwezi’ lakini tupo vizuri kiuchumi na tukishikana kwa pamoja uchumi wetu utapaa vizuri sana”