Rais Samia amesema hayo leo Kagera wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge ambapo amesema “Tumewekeza pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo, tunaamini Viongozi wa ngazi zote watasimamia matumizi sahihi ya fedha hizo, inasikitisha kuona kuna Watu hawajali na hawahurumii Wananchi, wanawapa miradi Makandarasi wasio na uwezo, Wala rushwa, Wezi na Wazembe wanaosababisha miradi kutotekelezwa”- Rais Samia
“Yanatokea haya Viongozi tukiwa tupo katika ngazi zetu tofauti, tunaona ila tunasubiri Vijana Wakimbiza Mwenge ndio waje waseme kama miradi ni mibovu na hailingani na thamani ya fedha iliyotumika, huu sio mtindo mzuri, nawaagiza wale wote walio kwenye nafasi za Mamlaka kusimamia fedha za Wananchi, hii ni kodi ya Wananchi inayoshushwa kwa ajili ya maendeleo yao na ni vema ikasimamiwa vizuri”– Rais Samia