Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amehutubia Wananchi wa Longido katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo tarehe 18 Oktoba, 2021 katika Uwanja wa stendi mpya Longido Mkoani Arusha.
“Niliona bango linadai Mji wa Namanga, masuala haya yana vigezo vyake kwa sasa hivi Namanga bado haijakidhi vigezo lakini pia katika kudai Mji Mdogo fuateni hatua kwa hatua kila jambo lina taratibu zake”- Rais Samia
“Lakini tukiitoa Namanga kuifanya Mji Mdogo mnaiua Longido, tusubirini tuongeze vyanzo vya mapato maendeleo yaonekane halafu tutafikiria hayo mambo baadaye lakini kwa sasa naomba mbaki kama mlivyo”——— Rais Samia akiwa Longido
“Nihimize katika kufanya kazi kwenu masuala ya nidhamu Longido hapa kulikuwa na Mkurugenzi mkorofi sana, hakukuwa na nidhamu ya kufanya kazi na ndio maana nikamtoa Longido nikampeleka kwingine akajifunze na hilo kumuhurumia tu ilikuwa nimuache kabisa”
“Kwahiyo niwahimize wote mnaofanya kazi katika ngazi ya Wilaya na hata ngazi za Mkoa kuheshimiana na nidhamu ya kazi, kila Mtu ana mamlaka yake muheshimiane nidhamu iwepo mfanye kazi kwa ushirikiano na maendeleo yatakuwepo”——— Rais Samia akiwa Longido