Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy yuko salama baada ya gari kugonga msafara wake mjini Kyiv, msemaji wake Serhii Nykyforov amethibitisha kupitia ukurasa wake wa FaceBook mapema Alhamisi.
Zelenskyy alikuwa akirejea katika mji mkuu baada ya ziara ya kushtukiza huko izyum, mji muhimu uliorejeshwa chini ya vikosi vya Ukraine baada ya jeshi ya Urusi kurudi nyuma.
Nykyforov amesema Zelenskyy hajapata “majeraha makubwa.’
“Gari liligongana na gari la rais na magari yake ya kusindikiza huko Kyiv,” msemaji wa Zelenskyy alisema.
“Rais alichunguzwa na daktari, hakuna madhara makubwa.” Madaktari waliokuwa wakiandamana na
Zelenskyy walimpa dereva wa gari hilo msaada wa dharura, kabla ya kumhamishia gari la wagonjwa.
Nykyforov hakusema ni muda gani ajali hiyo ilitokea.