Rais wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said @caamil_88 amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) @psg ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2023.
Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.
Vilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0.





