Rais wa Zambia, Edgar Lungu amemfuta kazi waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya ambaye mwezi Juni mwaka jana alikamatwa kwa tuhuma za rushwa kabla ya kufutiwa tuhuma hizo.
Chilufya amekuwa akikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo rushwa ya $17m (takribani shilingi bilioni 40) iliyohusisha usambazaji wa glovu za upasuaji na mipira ya kuzuia mimba.
Hata hivyo Ikulu ya Zambia haijatoa maelezo ya sababu za kufutwa kazi kwa waziri huyo huku kiongozi wa upinzani nchini humo Hakainde Hichilema akisema hatua hiyo “imechelewa mno”.